Thursday, February 22, 2018

KATA YA TOMONDO YAPATA NEEMA

Kiongozi waChama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, akiwa katika darasa la Shule ya Msingi Vuleni iliyoko Kata ya Tomondo jimbo la Morogoro Kusini alipotembelea shule hiyo jana, kuangalia miradi inayosimamiwa na diwani wa Chama hicho, ambako kiongozi huyo aliahidi kutoa bati za madarasa mawili.
Kiongozi waChama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe (kulia), akiwa na diwani wa chama hicho, Hamisi Msangule (kulia) pamoja na viongozi wa ngazi mbalimbali wa chama hicho wakitoka kwenye darasa la Shule ya Msingi Vuleni iliyoko Kata ya Tomondo jimbo la Morogoro Kusini alipotembelea shule hiyo jana, kuangalia miradi inayosimamiwa na diwani wa Chama hicho, ambako kiongozi huyo aliahidi kuchangia bati za madarasa mawili.
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe (katikati), akiwa na viongozi wa chama hicho wa Mkoa wa Morogoro na Jimbo la Morooro Kusini Mashariki kwenye eneo la mto Lugwazi ambako mradi wa barabara utapita kwa kumwagwa zege kwenye eneo hilo, ambako Chama hicho kimechangia mifuko 20 ya saruji kati ya 60 inayohitajika.
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe akiwa kwenye usafiri wa bodaboda wakati akienda kukagua miradi ya maendeleo ya Kata ya Tomondo Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki jana.
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe na Viongozi wa chama hicho mkoa wa Morogoro Wilaya na Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki wakimsaidia mkazi wa Kijiji cha Vuleni kuandaa mahindi wakati wakiwa kwenye ziara ya kukagua miradi yamaendeleo kwenye kata ya Tomondo inayoongozwa na chama hicho.
Viongozi wa Chama cha ACT Wazalendo wakiongozwa na Zitto Kabwe kuangalia chanzo cha maji kinachotumika na wakazi wa Kijiji cha Vuleni Kata ya Tomondo ambako chama hicho kimeahidi kuchimba visima virefu kila Kijiji haraka iwezekanavyo.
…………………

WAKAZI wa kata ya Tomondo wilayani Morogoro jimbo la Morogoro Kusini Mashariki wiki hii imekuwa ni ya neema kwao kutokana na kupata ufumbuzi wa baadhi ya kero za miradi yao mbalimbali ya maendeleo.

Kata hiyo inayoongozwa na diwani wa chama cha ACT Wazalendo, Hamisi Msangule jana ilitembelewa na viongozi wa chama hicho ngazi ya Taifa, Mkoa na Jimbo ambao waliwezesha kutatua baadhi ya changamoto za maendeleo.

Changamotokubwa ambayo imepewa kipaombele kutatuliwa na chama hicho ni kero ya maji inayowakabili wakazi wa kata hiyo ambayo chama hicho imeahidi kuwapeleka wataalamu wa kutoboa visima virefu kwenye kila Kijiji ndani ya mwezi huu.

Akizungumza kwenye kikao cha ndani na wananchi wa kata hiyo jana Kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe aliwaambia wananchi hao kama watashindwa kumaliza kero hiyo haitakuwa na aana tena chama hicho kupewa dhamana tena kuongoza.

“Chama chetu ni tofauti sana na vyama vingine, tunafanya siasa za maendeleo kwa ushirikishaji wananchi katika kutatua changamoto zao, alisema.

Mbali ya ahadi ya kumaliza kero ya maji kiongozi huyo pia amechangia mifuko ishirini ya saruji kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa barabara inayokatiza kwenye mto Lugwa kwenye Kijji cha Vuleni.

Neema iliendelea kuwaangukia Kijiji cha vuleni baada ya Kiongozi huyo kuahidi kuchangia bati zote zitakazo hitajika kukamilisha ujenzi wa madarasa mawili kati ya saba yanayohitajika shuleni hapo, yatakapoanza kujengwa.

Awali akitoa maelezo kwa Kiongozi huyo, diwani wakata hiyo, Hamisi Msangue alisema, Kata hiyo kwakuwa ni mpya ina changamoto nyingi hivyo kunahitajika nguvu nyingi ili kuweza kufanikisha maendelo na kutekeleza ahadi walizoahidi wananchi.

Diwani huyo aliwaeleza viongozi wa chama hicho kuwa zahanati yao ina manesi wawili tu na haina mganga jambo linalowaletea usumbufu wa kupata huduma za afya kwa wananchi.

Aidha changamoto nyingine nyingi zilielezwa kuwa zinahitaji ufuatiliaji kwa mamlaka zinazohusika kwaajili ya kupata majibu na kuahidi kupeleka mrejesho haraka iwezekanavyo.

Kata hiyo kama zilivyo kata nyingi za mkoa wa Morogoro nayo haikuachwa nyuma kwenye migogoro ya aridhi, kutokana na wanachi wengi kumlalamikia mwekezaji wa kizungu anaemiliki hekta 600 za Kijiji hicho bila ya kufata taratibu.

Ziara za Chama hicho kukagua maendeleo kwenye kata zinazoongozwa na madiwai wa chama hicho zinaendelea.

No comments: