Monday, July 31, 2017

MAKAMU WA RAIS AZINDUA MPANGO MKAKATI WA WATER AID TANZANIA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa Water Aid Tanzania kwa mwaka 2016-2021 wenye kauli mbiu "Kuweka Maji na Usafi wa Mazingira kuwa kitovu cha Maendeleo"iliyofanyika  kwenye hotel ya HyattRegency jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Gerson Lwenge wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa Water Aid Tanzania kwa mwaka 2016-2021 wenye kauli mbiu "Kuweka Maji na Usafi wa Mazingira kuwa kitovu cha Maendeleo"iliyofanyika  kwenye hotel ya HyattRegency jijini Dar es Salaam. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mohamoud Thabit Kombo wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa Water Aid Tanzania kwa mwaka 2016-2021 wenye kauli mbiu "Kuweka Maji na Usafi wa Mazingira kuwa kitovu cha Maendeleo"iliyofanyika  kwenye hotel ya HyattRegency jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyesha kitabu maalumu chenye mpango mkakati wa Water Aid ​

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassana leo amezindua Mpango Mkakati wa Water AID Tanzania .
Katika mkutano huo uliofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Gerson Lwenge, Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo, Mkurugenzi wa Water Aid Kanda ya Afrika Mashariki Bi. Olutayo Bankole –Bolawole,Mkurugenzi WaterAid Tanzania Dkt. Ibrahim Kabole na wadau mbali mbali wa maji, afya na mazingira.
Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Water Aid Tanzania wenye lengo la “ Kuweka Maji Safi na Usafi wa Mazingira (WASH)” katika mipango ya Maendeleo ya Jamii.
Makamu wa Rais aliwapongeza  Water Aid Tanzania kwa mpango wake huo, alisema Maji ni rasilimali ambayo haijawahi kutosheleza  mahitaji ya dunia na hapa kwetu pia kwani kuna mahitaji makubwa ya maji kwa ajili ya shughuli za kijamii, kiuchumi na kuhuisha na kutunza mazingira.
Vilevile  vyanzo vya maji vinaathiriwa sana na Ukame,kufurika n, kuvuruga mtiririko asilia, mabadiliko ya hali ya hewa ongezeko la idadi ya watu na viumbe wengine (Wanyama).
Mpango wa Water Aid Tanzania wa miaka mitano  utawezesha kuiweka Tanzania kwenye ramani ya matumizi endelevu ya rasilimali ya maji na utachangia katika utekelezaji wa malengo tuliyojiweka ya kupeleka huduma ya maji safi na salama kwa wananchi kulingana na Sera yetu ya Maji na pia kutekeleza ahadi tulizozitoa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya 2015.
Makamu wa Rais alisema Serikali kwa kushirikiana na wadau mbali mbali imeendelea kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika maeneo ya vijijini ambapo utekelezaji huo umeendelea kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji vijijini ambapo kwa mwezi Juni 2017 jumla ya watu 22,952,371 sawa na asilimia 72.58 ya wananchi waishio vijijini wanapata maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kama sera ya maji ya mwaka 2002 inavyoelekeza huku katika Miji Mikuu  ya mikoa kutoka asilimia 86 hadi asilimia 95, katika miji mikuu ya Wilaya , miji midogo na miradi ya Kitaifa kutoka asilimia 60 hadi asilimia 75 na katika jiji la Dar es Salaam kutoka asilimia 72 hadi asilimia 95 ifikikapo 2020.
Makamu wa Rais alisisitiza suala la usafi wa mazingira na kuhakikisha tunalinda afya zetu tusishambuliwe na magonjwa ya milipuko kama  vile kipindu pindu na homa za matumbo.  “Sote tunajukumu kubwa kuhakikisha tunapata maji na kuzungukwa na Mazingira safi”.
Makamu wa Rais aliwaagiza wanaohusika na usimamizi wa miradi ya maji na usafi wa mazingira kuongeza jitihada zaidi ifikapo 2020 idadi ya wananchi wanaopata maji iwe imeongezeka kufikia malengo tuliyojiwekea.
Mwisho, Makamu wa Rais aliwashukuru wawakilishi wa mashirika yote ya Maendeleo, wafadhili binafsi na Watendaji wengine ikiwa pamoja na Sekta Binafsi na Taasisi za Kidini ambazo zimesaidia katika upatikanaji wa huduma za maji na usafi wa mazingira na kuboresha mazingira.

No comments: