Friday, July 31, 2015

VIJANA WAJASILIAMALI ZAIDI YA 650 WAKWAMLIWA KIUCHUMI NA AIRTEL FURSA

 Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Solution Blocks, Msomisi Mbenna akiwakaribisha wageni katika semina ya kuhamasisha makampuni mbalimbli  kukabiriana na ukosefu wa ajira hapa nchini ili kumwezesha kijana mjasiliamali kujikwamua kiuchumi katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam jana.
 Wageni kutoka makampuni mbalimbali wakimsikiliza  Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Solution Blocks, Msomisi Mbenna katika mkutano wa ajira kwa vijana wajasiliamali wanaothubutu kujikwamua kiuchumi hapa nchini katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam. 
Meneja wa huduma za jamii-Airtel Hawa Bayuni akielezea jinsi kampuni la airtel  hapa nchini linavyoendelea kukomboa vijana wajasiliamali wanathubutu kujikwamua kiuchumi hasa kwa kutumia Aitel Fursa inayoendelea kuwawezesha vijana wengi hapa nchini wa kuanzia miaka 18 hadi 24 ikiwa Aitel fursa imeshasaidia vijana wajasiliamali zaidi ya 650 kwa mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza na Arusha ikiwa inaendelea kwa mikoa mingine hapa nchini.katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam. 
 Baadhi ya washiriki wa Mkutano ulioandaliwa na kampuni ya Solution Blocks wakimsikilizaMeneja wa huduma za jamii-Airtel Hawa Bayuni akielezea jinsi AIRTEL FURSA ilivyokwamua changamoto mbalimbali kwa vijana wajasiliamali hapa nchini waliokua na malengo ya kujikwamua kiuchumi kwa kuwapa vifaa pamoja na kuwasaidia kimasoko.
 Mwenyekiti wa kampuni ya  Roots and Shoot, Ray Kiliho akichangia maada katika mkutano ulioandaliwa na kampuni ya Solution Blocks baada ya mtoa maada kutoka kampuni ya simu za mkononi Airtel Hawa Bayuni kuhusiana na changamoto zinazomkuta kijana mjasiliamali wakati wa kuendeleza biashara yake, katika mkutano uliofanyika katika hoteli hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Solution Bloks, Msomisi Mbenna akiuliza swali kwa Meneja huduma za jamii wa Airtel  hapa nchini ,Hawa Bayuni katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam.
 Mwakilishi wa kampuni ya Popular lines, Neserian Alexander akichangia maada mara baada ya mtoa maada kumaliza kuelezea jinsi Airtel Fursa inavyoendelea kukwamua vijana kiuchumi hapa nchini katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa hoteli ya Colossem, Tanya Visser akitoa zawadi kwa washiriki wa mkutano ulioandaliwa na kampuni ya Solution Blocks uiofanyika jana jijini Dar es Salaam. 




Washiriki wa mkutano ulioandaliwa na kampuni ya Solution Blocks  wakiwasikiliza watoa maada kutoka Airtel  na kampuni ya Solution Blocks  katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam.

No comments: