Sunday, August 31, 2014

Wabunge Afrika Mashariki watembelea Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa)

 Spika wa Bunge la Jumuiya ya AfrikaMashariki (EALA) Mhe. Margareth Zziwa akipanda mti  katika eneo la Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) jana wakati wa ziara ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Upandaji wa mti huo ni katika kutekeleza azimio la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika jitihada za kutunza mazingira
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na  Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) akipanda mti  katika eneo la Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) jana wakati wa ziara ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Upandaji wa mti huo ni katika kutekeleza azimio la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika jitihada za kutunza mazingira.
 Spika wa Bunge la Jumuiya ya AfrikaMashariki (EALA) Mhe. Margareth Zziwa (Kulia) akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi wa  Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) tayari kwa kuonyesha na kuuza bidhaa zao wakati wa ziara ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotembelea Taasisi hiyo jana mjini Bagamoyo. 
 Mmoja wa wabunge wa Bunge la Jumuiya ya AfrikaMashariki (EALA) Mhe. Susan Nakawuki (mwenye blauzi ya pinki) akinunua bidhaa kutoka kwa mmoja wa wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi wa  Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) tayari kwa kuonyesha na kuuza bidhaa zao wakati wa ziara ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotembelea Taasisi hiyo jana.
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) akiweka saini katika daftari la wageni katika moja ya kikundi cha wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi wa  Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) tayari kwa kuonyesha na kuuza bidhaa zao kwa wakati wa ziara ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotembelea Taasisi hiyo jana.
 Baadhi ya Wabunge wa Afrika Mashariki akiwemo Mhe. Shyrose Bhanji anayewakilisha  Tanzania katika bunge hilo wakiangali kazi za sanaa ya uchingaji kutoka kwa mmoja wa wajasiriamali waliokuwa wameweka bidhaa zao nje ya ukumbi wa  Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) tayari kwa kuonyesha na kuuza bidhaa zao kwa wakati wa ziara ya Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliotembelea Taasisi hiyo jana.
 Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Shyrose Bhanji wa Tanzania akimkabidhi zawadi ya sinia lililotokana na kazi za uchongaji Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Margareth Zziwa mara baada ya kupenda bidhaa hiyo na kuamua kumnunulia spika huyo jana wilayani Bagamoyo wakati wa ziara ya Wabunge wa Afrika Mashariki katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa).
 Katikati ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki ambaye pia ni mtoto wa Baba wa Taifa Mhe. Makongoro Nyerere (katikati) akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afika Mashariki wa  Serikali ya Tanzania Bibi. Joyce Mapunjo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel walipokuta katika viwanja vya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) wakati wa ziara ya wabunge wa Afrika Mashariki katika Taasisi hiyo.
 Spika wa Bunge la Jumuiya ya AfrikaMashariki (EALA) Mhe. Margareth Zziwa (Kulia) akikabidhi kitabu cha mpango mkakati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa  Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) Bw. Michael Kadinde wakati wa ziara ya Wabunge wa Afrika Mashariki. TaSuBa ni taasisi pekee katika ukanda wa Afrika Mashariki uliopewa dhamana ya kuwa Kituo cha Maarifa katika Nyanja za Sanaa na Utamaduni
 Spika wa Bunge la Jumuiya ya AfrikaMashariki (EALA) Mhe. Margareth Zziwa (Kulia) akikabidhi kitabu cha mpango mkakati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe Ahmed Chipozi jana wilayani Bagamoyo wakati wa ziara ya Wabunge wa Afrika Mashariki katika taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSuBa). Anayeshuhudia katikati ni Waziriwa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB).
 Spika wa Bunge la Jumuiya ya AfrikaMashariki (EALA) Mhe. Margareth Zziwa (Kushoto)  na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB).wakiwa na baadhi ya Wabunge wa Afrika Mashariki wakipata maelezo kuhusu muelekeo na malengo ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa)  kutoka Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo Bw. Michael Kadinde jana wakati wa ziara ya wabunge hao.
 Kikundi cha Sanaa kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSuBa)wakifanaya sanaa za maonyesho kwa mchezo aina ya  Akrobati mbele ya wageni ambao ni wabunge wa Afrika Mashariki wakiongozwa na Spika wa Bunge hilo Mhe. Margareth Zziwa (Hawapo picha) walipotembelea taasisi hiyo jana mjini Bagamoyo.
 Kikundi cha Sanaa kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSuBa)wakichezo ngoma yenye asili ya kabila la Kisukuma ijulikanayo kama Gobogobo mbele ya wageni ambao ni wabunge wa Afrika Mashariki wakiongozwa na Spika wa Bunge hilo Mhe. Margareth Zziwa (Hawapo picha) walipotembelea taasisi hiyo jana mjini Bagamoyo.
 Baadhi ya wageni wakifurahia ngoma wakati wa ziara ya wabunge wa Afrika Mashariki jana mjini Bagamoyo walipotembelea Tasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa).
Kutoka kulia mwenye skafu niNaibu Waziri wa Afrika Mashariki wa Tanzania Dkt.Abdulla Juma Abdulla, Spika wa Bunge la Jumuiya ya AfrikaMashariki (EALA) Mhe. Margareth Zziwa (mwenye miwani), Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB), Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Makongoro Nyerere, Mwenyeki ti wa Bodi wa TaSuBa Bw. Abraham Bafadhili na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TaSuBa Bw. Michael Kadind wakiwa katika picha ya pamoja na wasanii wa kikundi cha sanaa kutoka taasisi hiyo wakti wa ziara ya wabiunge wa Afrika Mashariki katika taasisi hiyo jana.

No comments: