Wednesday, April 30, 2014

Misokoto ya bangi 2,676 yakamatwa Manyara; watuhumiwa waendelea kupeta mtaani!

 JESHI la Polisi hapa nchini, limeshindwa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa madawa ya kulevya katika mkoa wa Manyara, ambapo kwa sasa Polisi wamekamata misokoto ya bangi 2,676 na mirungi bunda 70 katika mkoa huo, huku likishindwa kakabiliana na hali hiyo kutokana na Askari wake kushiriki vitendo hivyo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Bangi1
Aidha kumbukumbu zinaonyesha kuwa katika kipindi cha Machi, mwaka 2012, Jeshi hilo mkoani Kilimanjaro lilimshikilia Askari wake (G 842, Konstebo Deogratius), ambaye alikamatwa na misokoto mine ya bangi akiwa katika ukumbi wa disko wa Albeto uliopo mjijni Moshi, huku akifanya vurugu katika ukumbi huo ambapo pamoja na Jeshi la Polisi mkoani humo kuthibitisha tukio hilo, mtuhumiwa huyo akisukwa rumande pamoja na Askari mwingine ambaye aliingia katika ukumbi huo akiwa na bunduki aina ya SMG na kufanyia watu fujo.

Mbali na matukio hayo Jeshi hilo, lilitoa taarifa ya kukamata kwa watuhumiwa 45 wakihusishwa na matukio ya utumiaji wa bangi, mirungi na gongo katika msako wa kuimarisha doria katika maeneo mbalimbali mkoani humo, msako ambao hadi leo Polisi mkoani humo wameshindwa kuwafikisha makahamani watuhumiwa wakidai bado uchunguzi haujakamilika Globu ya Jamii imebaini.

bangi watuhumiwa

Misokoto 2,676 ya bangi yakamatwa


Kamanda wa Polisi mkoani humo, Deusdedit Nsimeki, amemwambia Mwandishi wetu kuwa Aprili 15 saa 11:30 asubuhi katika eneo la Minjingu barabara ya Arusha-Babati, walimkamata, Nassoro Idd (27) mburege mkazi wa Singida mjini akiwa na misikoto ya bangi 2000 akiwa anatumia usafiriwa basi la kampuni ya Mtei lenye namba T.449 CAL, lililokuwa likitokea Arusha kwenda Singida.

Amesema siku hiyo hiyo huko minjingu Kata ya Nkaiti, Askari waliokuwa doria walimkamata, Juma Khatibu (18) Mshilazi na mkulima wa Arusha, akiwa na bangi misokatomo 620, iliyokuwa imehifadhiwa ndani ya mikate iliyokuwa imetobolewa, ambapo mtuhumiwa alikuwa ni abiria wa basi la kampuni ya Kandahar lenye namba T. 391 BUR lililokuwa likitokea Moshi kwenda mkoani Singida.

Bangi msokoto
Aidha Nsimeki, alisema katika Kata ya Nkaiti, wilayani Babati, Riziki Ferisi (18) Mchaga na mkulima wa moshi alikutwa na bangi misokoto 56 akiwa kwenye basi la Mtei lenye namba T.991 ABC, lililokuwa likitokea Moshi kwenda Singida, ambapo Aprili 13 maeneo ya magugu, Edward Mollel (27), Janeth Mollel (27 na Mudi Robert (33) kwa pamoja walikuwa wanasafirisha madawa ya kulevya aina ya Mirungi bunda 70 yaliyokuwa kwenye gari aina ya Noah yenye namba T.339 BYE, inayomilikiwa na Edward Mollel, mkazi wa Singida.

“Pamoja na kuwa kuna mbinu mpya zinatumika kusafirisha madawa haya, ikiwemo kuweka kwenye siti za magari kama Noah,’Tyubu’ za matairi ya magari, mifuko mbalimbali na mabegi, na kuweka ndani ya mikate iliyotobolewa lakini bado tumegundua mbinu hizo” alisema Nsimeki.

Ameiambia FikraPevu kuwa, Jeshi hilo limejizatiti kwa kuhakikisha kuwa hakuna makosa ya uhalifu, yatakayovunja amani katika maeneo yote ya mkoa huo katika kipindi hiki cha sikukuu za Pasaka.

Walimiki wa mabasi kukumbana na mkono wa sheria

Sanjari na watuhumiwa hao kukamatwa,Jeshi hilo limesema litachukua hatua kwa wamiliki wa mabasi, ambayo yatapatikana na madawa hayo yakiwemo yaliyokamatwa katika zoezi hilo, huku akitoa wito kwa wananchi wa mkoa huo kutoa ushirikiano wa dhati kwa Jeshi hilo, ili kuwabaini watuhumiwa mablimbali.

No comments: