Friday, May 31, 2013

NSSF MEDIA ALL STARS Vs WABUNGE LIVE ON STAR TV

 Kocha wa timu ya NSSF Media All Stars, Sanifu Lazaro akipimwa afya na Dk. Frida Francis kutoka Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo kabla ya kuanza kwa safari ya kwenda Dodo kupambana na timu ya Wabunge siku ya Jumamosi Juni Mosi kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma. Pambano hilo litaoneshwa Live kupitia Star Tv.
 Dk. Margreth Mtaki kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo akimpima afya mshambuliaji wa timu ya soka ya NSSF Media Kombaini, Maulid Kitenge kabla ya safari ya kwenda Dodoma kupambana na timu ya Wabunge. 
 Mchezaji wa timu ya Netiboli ya NSSF Media Kombani, Somoe Ng'tu akipimwa afya. 
 Majuto Omari akipimwa afya.
 Salum Mkandemba akichukuliwa vipimo vya afya.
 Wachezaji wa timu ya Netiboli ya NSSF Media All Stars wakiwa katika mazoezi ya lkujiandaa na mnchezo wao dhidi ya Wabunge.
 Wachezaji wa timu ya NSSF Media All Stars wakiwa katika mzoezi ya kujiandaa na mchezo wao kwenye Uwanja wa TCC Chang'ombe jijini Dar es Salaam.
 Mazoezi ya viungo
 Kocha wa NSSF Media All Stars, Sanifu Lazaro (kulia) akiongoza mazoezi ya timu hiyo.
 Mbinu za ushindi.
 Kiongozi wa msafara wa timu ya NSSF Media All Stars, Juma Kintu (kushoto) akibadilishana mawazo na mchezaji wa timu hiyo, Linus Bugogwa, wakati wa mazoezi ya timu hiyo kwenye uwanja wa TCC Chang'ombe jijini Dar es Salaam. Timu hiyo imeindoka leo kwenda mjini Dodoma kupambana na timu ya wabunge.
 Wachezaji wa timu ya NSSF Media All Stars wakijifua kwa ajilki ya mchezo wao dhidi ya Wabunge.
 Maandalizi ya mchezo.
 Kiongozi wa msafara wa timu ya NSSF Media All Stars, Juma Kintu akitoa maelekezo kwa wachezaji wa timu ya Netiboli ya NSSF Media All Stars baada ya mazoezi yao ya mwisho kabla ya safari ya kwenda Dodoma kukipiga na timu ya Wabunge. 

No comments: