Friday, March 29, 2013

HIVI NDIVYO MAMBO YALIVYO ENEO LA JENGO LILILOPOEROMOKA LEO


Hivi ndivyo lionekanavyo jengo hilo mara baada ya kuporomoka na asubuhi ya leo na kupelekea watu kadhaa kufukiwa na kifusi hicho wakiwepo watoto waliokuwa wakicheza mpira jirani na jengo hilo.
Watu wengi wakiwemo ndugu wa watu waliokuwepo kwenye jengo hilo wakiangalia hata ya kuokolewa kwa ndugu zao.
Juhudi za uokoaji zikiendelea japo kuna uhaba mkubwa sana wa vifaa vya uokoaji.
Moja ya Magreda yaliopo eneo hilo la tukio likiendelea na kazi  ya kutoa kifusi ili kurahisisha kazi ya uokoaji.
Kikukweli hali bado ni tete katika uokoani,maaka pia kuna ufinyu wa nafasi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick akiwasili eneo la tukio ili kuungana na waokoaji wengine kwenye zoezi hilo.
Watu wanajitahidi kwenye uokoani,lakini kuna uhaba wa vifaa vya uokoaji.
Mkuu wa Mkoa akisogea eneo la tukio.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Mh. Said Meck Sadick akipatiwa maelezo ya namna ya uokoaji kutoka kwa maafisa wa kikosi cha Uokoaji.
Wanajitahidi lakini wanakwamishwa na vifaa.
Wadau wakionyesha nondo zilizokuwa zimejengewa kwenye jengo hilo wakimaanisha kuwa hazina ubora.
Magari yaliyokuwepo jirani na jengo hilo yakiwa yameangukiwa na kifusi.
Kazi ikiendelea huku wengine wakiwa hawaani kilichotokea.
Mawasiliano ya hapa na pale yakiendelea kuhakikisha utaratibu wa uokoaji unafanikiwa.


Kikosi ya Msalaba mwekundu kipo eneo la tukio.
Ulinzi mkali.
Mdau akiwahisha ngazi kwa ajili ya kuendeleza zoezi zima la uokoaji.

Mpiga picha wa Magazeti ya Serikali ya Daily & Sunday News na Habari leo,Mohamed Mambo akiwajibika kuhakikisha anapata picha bora.
Kumbukumbu ikichukuliwa.


Mh. James Mbatia akijadiliana jambo na mmoja wa wadau walipo eneo la tukio.

9 comments:

Anonymous said...

POLENI SANA NYOTE MLIO KUMBWA NA AJARI,PIA POLE KWA WALIO FIWA NA NDUGU ZAO, PIA POLENI SANA MLIO JERUHIWA MUNGU ATAWAPONYA HARAKA.

PILI: KAZI KWA SERIKALI IFUATILIE KWA UNDANI NA KUWAKAMATA WAMILIKI NA MKANDARASI WA JENGO HILO. NA WOTE WALIO HUSIKA KATIKA KUSIGN MIKATABA NA KUMPATIA KAZI MKANDARASI HUYO. PIA NDUKA AU CAMPANY ILIYOKUWA IKIUZA VIFAA HIVYO VYA UJENZI PIA ICHUNGUZWE KWA UNDANI ZAIDI
nTAMABOY

Anonymous said...

POLEN TANZNIA

Anonymous said...

POLENI WOTE WALIOKUTWA NA MKASA HUU MKUBWA SIKU HII..INABIDI UFANYIKE PIA UKAGUZI WA UBORA WA MAJENGO YOTE YALIYO JENGWA KARIAKOO NA SEHEMU NYINGINE KOTE DAR ES SALAAM..MAANA TUNA TATIZO KUBWA LA MAKANDARASI NA UKAGUZI WA MAJENGO TANZANIA KWA UJUMLA..

Salva Sweke

Unknown said...

Poleni kwa yaliyowapata watanzania wenzangu na pole kwa walio poteza ndugu zao.

Unknown said...

Poleni watanzania wenzangu kwa yaliyowapata na pole kwa wote walio poteza ndugu zao

flora lyimo said...

SO SAD,,POLENI SANA NDUGU ZETUNI NIPO NANYI KATIKA SALA 'WALE WOTE WALIPOTEZA MAISHA YAO R.I.P NA WAGONJWA MPNO HARAKA,,AMEN"

Anonymous said...

Poleni sana watanzania wenzangu kwa msiba huu ni wetu sote.ila naomba selikari ichunguze kwa kina na wahusika wote washtakiwe pia kiwepo chombo cha wataalamu kila wilaya iwe inakagua majengo tangia linapoanza kujengwa pia vifaa vya ujenzi vikaguliwe kabla.

Anonymous said...

Inasikitisha sana na poleni sana watanzania wenzangu. Nina imani kwa hali hii watanzania tutaamka na kuanza kuwa serious tunapofuatilia jambo na kudai haki.

Anonymous said...

Poleni sana.