Friday, January 27, 2012

Mechi ya hisani kati ya Twiga Stars vs Bunge SC kwenye uwanja wa karume jijini dar

Kikosi cha timu ya Bunge SC kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wao na timu ya Taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’, ambao ulikuwa ni maalumu kuichangia timu hiyo uliofanyika kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. Twiga Stars imeshinda 2-1.
Kikosi cha Twiga Stars kikiwa katika picha ya pamoja.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi, akipeana mkono na mshambuliaji wa Twiga Stars, Mwanahamis Omari.
Wachezaji wa Bunge SC, Halima Mdee na William Ngeleja, wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza kwa mchezo.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu, akizungumza kabla ya kukabidhi kitita cha sh. milioni 7 kwa wachezaji wa Twiga Stars.
Nahodha wa timu ya Twiga Stars, Sophia Mwasikili, akionesha kitita cha sh. milioni 7 baada ya kukabidhiwa na Naibu Waziri, Ummy Mwalimu (kulia).
Mlinzi wa timu ta Twiga Stars, Siajabu Hassan akimtoka mshambuliaji wa Bunge SC, Adam Malima.
Mshambuliaji wa Bunge SC, Sadifa Juma Khamis akimtoka beki wa Twiga, Fatuma Khatib.
Mshambuliaji wa timu ya Bunge SC, Adam Malima akimtoka beki wa timu ya Twiga Stars, Siajabu Hassan wakati wa mchezo wa hisani  ambao ulikuwa ni ni maalumu kwa kuichangia timu ya Twiga Stars uliofanyika kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. Twiga Stars imeshinda 2-1.
Nahodha wa timu ya Twiga Stars, Sophia Mwasikili.Picha na Francis Dande.

1 comment:

Anonymous said...

All the best Twiga Stars..