Monday, October 31, 2011

UNFPA lasherehekea kilele cha dunia kufikisha watu bilioni 7,yatoa msaada wa vifaa mbalimbali hospitali ya Temeke jijini dar leo.

Dr . Julitta Onabanjo akiwapa pole na hongera kwa akina mama wazazi waliojifungua usiku wa kuamkia leo,kwenye hospitali ya Temeke,ambapo Dunia ilikuwa inatimiza idadi ya Watu bilioni 7
Dr . Julitta Onabanjo akiwa na akina mama 7 waliojifungua usiku wa kuamkia leo,ambapo kupitia shirika la mfuko wa idadi ya watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA)-Tanzania lilitoa msaada wa vitu mbalimbali kwa akina mama hao ikiwemo pia hospitali  hiyo kwa kupatiwa vifaa mbalimbali vya watoto.
Mgeni rasmi,ambaye pia ni muwakilishi wa shirika la mfuko wa idadi ya watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA)-Tanzania,Dr Julitta Onabanjo akiwa ameambatana na wenyeji wake wakiwa kwenye wodi ya Wanawake kwa ajili ya kutoa misaada kwa akina mama saba walijifungua usiku wa kuamkia leo,ambapo Dunia ilikuwa inatimiza idadi ya watu bilioni saba,na Tanzania ilikuwa inatimiza idadi ya watu bilioni 44.
 Mgeni rasmi pichani kati akiwa na wenyeji wake wakielekea kwenye wodi ya akina mama wazazi,kwa minajili ya kutoa msaada kwa wazazi saba waliojifungua watoto,ambapo dunia ilikuwa ikitimiza idadi ya watu bilioni 7.
 Mgeni rasmi,muwakilishi wa shirika la mfuko wa idadi ya watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA)-Tanzania,Dr Julitta Onabanjo akikabdhi sehemu ya msaada wa vifaa mbalimbali vilivyotolewa na shirika hilo kwa Dr. Heavengton Mshiu-MOHSWI RCH (Programe Officer- Safe Motherhood International), mapema leo asubuhi kwa ajili ya hospitali hiyo
Pichani Dr. Husna Msangi kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Temeke Hospitali jijini Dar,akimkabidhi hotuba fupi aliyokuwa akiisoma mbele ya Mgeni rasmi,ambaye ni muwakilishi wa UNFPA-Tanzania,Dr Julitta Onabanjo kwenye hafla fupi ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya hospitali hiyo,iliyofanyika mapema leo asubuhi,ambapo Dunia ilikuwa ikitimiza idadi ya watu bilioni 7.
Muwakilishi wa shirika la mfuko wa idadi ya watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA)-Tanzania,Dr . Julitta Onabanjo akifafanua jambo mapema leo asubuhi wakati hafla fupi ya kutoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa hospitali ya Temeke.
Pichani Dr. Husna Msangi kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Temeke Hospitali jijini Dar,akisoma hotuba fupi mbele ya Mgeni rasmi,ambaye ni muwakilishi wa UNFPA-Tanzania,Dr Julitta Onabanjo na wageni wengine waalikwa  mbalimbali waliokuwa wamefika (hawapo pichani) kwenye hafla fupi ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya hospitali hiyo,iliyofanyika mapema leo asubuhi,ambapo Dunia ilikuwa ikitimiza idadi ya watu bilioni 7.
 Pichani juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria kwenye hafla hiyo.

 
Kutoka kulia ni Dr. John Bwana- Kaimu Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke, Dr. Heavengton Mshiu-MOHSWI RCH (Programe Officer- Safe Motherhood International), Dr. Julitta Onabanjo ambae ni Muwakilishi Mkazi wa shirika la UNFPA- Tanzania, Syvia Mamkwe- Mganga mkuu wa Manispaa ya Temeke pamoja na Dr. Solanki Rajeshi- Dokta bingwa wa watoto- TMK Hospitali.
Pichani ni baadhi ya misaada mbalimbali iliyotolewa na shirika la mfuko wa idadi ya watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA)-Tanzania kwa hospitali ya Temeke.

No comments: