Monday, June 9, 2014

MAMIA WAMZIKA MSANII MKONGWE WA MAIGIZO NCHINI MZEE SMALL

 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili kwenye Msiba wa msiba wa msanii maarufu wa filamu ya vichekesho hapa nchini,Marehemu Saidi Ngamba “Mzee Small” nyumbani kwa marehemu Tabata Kimanga jijini Dar es salaam leo Juni 9, 2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika dua wakati alipokwenda kuhani msiba wa msanii maarufu wa filamu vichekesho Marehemu Saidi Ngamba “Mzee Small” nyumbani kwa marehemu Tabata Kimanga jijini Dar es salaam leo Juni 9, 2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwafariji wafiwa wakati walipokwenda kuhani msiba wa msanii maarufu wa filamu vichekesho Marehemu Saidi Ngamba “Mzee Small” nyumbani kwa marehemu Tabata Kimanga jijini Dar es salaam leo Juni 9, 2014
Mama Salma Kikwete akimpa pole mjane wa Marehemu Saidi Ngamba “Mzee Smal” wakati alipokwenda kuhani msiba wa msanii huyo maarufu wa filamu za vichekesho nyumbani kwa marehemu Tabata Kimanga jijini Dar es salaam leo Juni 9, 2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amejumuika na waombolezaji mbali mbali kwenye Msiba wa msanii maarufu wa filamu za vichekesho nyumbani kwa marehemu Tabata Kimanga jijini Dar es salaam leo Juni 9, 2014.Kusoto ni Rais wa Chama cha Filamu nchini,Simon Mwakifwamba na kulia ni Mtoto wa Marehemu Mzee Small,Mahmoud Said Ngamba.
Rais Kikwete akisaini Kitabu cha Maombolezo.
Dua zikiendelea kusomwa kumuombea Marehemu Said Ngamba "Mzee Small". 
Rais Kikwete akielezwa jambo na Bw. Mwakifwamba.
 MC Mkelle akiongoza shughuli ya Msiba huo.
Waombolezaji Msibani.
 
 Mtoto wa Marehemu Mzee Small,Mahmoud Said Ngamba akionekana ni mwenye Majonzi sana.
 Mmoja kati ya watu waliofanya kazi nyingi na Marehemu Mzee Small,Bwana Tupatupa akiongea na vyombo vya habari.
 Rais Kikwete akiagana na Mtoto wa Marehemu Mzee Small,Mahmoud Said Ngamba.
 Rais Kikwete akiwaaga waombolezaji msibani hapo.

Mama Salma Kikwete akiondika msibani hapo baada ya Kuhani msiba huo.

 Waombolezaji msibani.
 Jeneza likipakiwa kwenye gari tayari kwa safari ya Mazikoni.
 Msafara wa magari na waendesha Bodaboda wakiwa katika barabara ya Segerea Kinyerezi wakati wakielekea Makaburi ya Segerea kwaajili ya Kumpumzisha Kwa Amani Mkongwe wa Sanaa ya Vichekesho Nchini Said Ngamba almaarufu Mzee Small
 Gari lililobeba Mwili wa Marehemu Said Ngamba aka Mzee Small (la kwanza) likiwa limesimama kwaajili ya Vijana kuubeba Mwili wake hadi kwenye Makaburi ya Segerea jioni Hii
 Vijana wakishusha jeneza lenye mwili wa Marehemu Mzee Small kwaajili ya kuelekea kwenye Makaburi ya Segerea
 
Vijana wakiwa wamepanga mstari kuanzia Barabara ya Segerea Kinyerezi hadi makaburini kwaajili ya kupokea jeneza lenye Mwili wa Marehemu Mzee Small
 Vijana wakiwa wamebeba jeneza lenye Mwili wa Marehemu Mzee Small wakielekea kwenye Makaburi ya Segerea Jioni Hii.
 Watu mbalimbali wakisubiri Mwili wa Marehemu kuwasili katika makaburi ya Segerea
 Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Simon Mwakifamba akiwasilika katika eneo la Makaburi ya Segerea jioni hii kwaajili ya kumzika Mzee Small
 Mwili wa Marehemu Mzee Small ukitolewa kwenye jeneza tayari kupumzishwa katika Nyumba yake ya Milele katika makaburi ya Segerea.
 Watu mbalimbali wakiwasili kwenye makaburi ya Segerea kwaajili ya kumzika Mzee Small. Picha Zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog 
 Umati wa watu wakielekea Kupokea Jeneza lenye mwili wa Marehemu Mzee Small wakati ulipowasili kwenye eneo la Makaburi ya Segerea.
 Wanahabari wakitafuta taswira katika mazishi ya Mzee Small katika Makaburi ya Segerea
Picha Zote na Othman Michuzi, 
Francis Dande na Josephat Lukaza.
MAMIA ya wakazi wa jijini Dar es Salaam, jana walijitokeza kwa wingi katika kumsindikiza gwiji wa vichekesho nchini, Said Ngamba ‘Mzee Small’ katika safari yake ya mwisho, ambako alizikwa jana jioni katika makaburi ya Segerea jijini Dar es Salaam.

Aidha, Rais Jakaya Kikwete, alifika nyumbani kwa marehemu Tabata, kuwapa pole wafiwa, ndugu, jamaa na marafiki.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa maziko, Muigizaji mkongwe, Bakari Mbelemba ‘Mzee Jangala’ alisema Mzee Small ni mfano wa kuigwa katika tasnia ya uigizaji na wataendelea kumkumbuka na kumuenzi, huku akiwaasaa wasanii chipukizi kuiga mazuri yake.

Naye Rais wa Bongo Movies, Steve Nyerere, alizidi kuwaasa wasanii vijana kupenda na kufuata nyazo za wakongwe hao tofauti na hali ilivyo hivi sasa, ambako chiku na dharau zimekuwa zikitawala.

Steve alikwenda mbali zaidi na kudai, kifo cha Mzee Small kimewaweka kwenye hali ngumu, kwani wakati akiugua, wasanii wa Bongo Movies walikuwa wazito kumjulia hali na hata kutoa msaada, jambo wanalolijutia.

Mzee Small aliyezaliwa mwaka 1955 katika Kijiji cha Kililima, Kilwa mkoani Lindi, alifariki dunia Juni 7 katika Hospitali ya Taifa Muhumbili alikokuwa amelezwa.
 Ngugu jamaa na marafiki wakishiriki mazishi ya msanii wa maigizo, vichekesho marehemu, Said Ngamba maarufu kama mzee small katika makauri ya Segerea jijini Dar es Salaam, leo. 
 Baadhi ya waombelezaji wakiwa wamebeba  jeneza lililokuwa na mwili wa msanii wa Maigizo ya Vichekesho, Said Ngamba ‘Mzee Small’ wakati wa kuelekea kwenye makaburi  ya Tabata Segerea jijini Dar es Salaam.
Safari ya mwisho ya mzee Small.
Mazishi ya mzee Small.
 Nyota wa filamu wakibadilishana mawazo
 Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa Godfrey Mngereza katikati akiwa na Mzee Chiro msanii wa filamu kushoto ni Teacher 

Msanii Ray akiwa na waombolezaji wenzie

No comments: